# Yahwe atajulikana kwa Misri Hapa "Misri" ina maana ya watu wa Misri. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawafanya watu wa Misri kumjua" # watamtambua Yahwe "watapokea ukweli juu ya Yahwe" au "watakubaliana na ukweli juu ya Yahwe" # Watamwabudu Kitu cha ibaada yao kinaweza kuwekwa wazi. "Watamwabudu Yahwe" # watatoa viapo kwa Yahwe na kuzitimiza '"watatoa ahadi kwa Yahwe na kuzishika" au "'watatoa ahadi kwa Yahwe na watafanya kile walichokiahidi kufanya" # Yahwe ataiumiza Misri Hapa, "Misri" ina maana ya watu wa Misri. "Yahwe ataumiza watu wa Misri" # umiza "kupiga" au "kuadhibu" # kuwaumiza na kuwaponya Neno "wao" linaeleweka katika msemo huu. "kuwaumiza wao na kuwaponya wao" # kuwaumiza na kuwaponya Jinsi msemo huu unavyohusiana na msemo kabla yake unaweza kuwekwa wazi kwa maneno '"baada" na "pia". "na baada yake kuwaumiiza, pia atawaponya"