# wamefanya Misri ipotoke, ambayo ni jiwe la pembeni la makabila yake Wakuu wa Soani na Nofu wanazungumziwa kana kwamba wao ni jiwe la pembeni la majengo kwa sababu wao ni sehemu muhimu katika jamii. "viongozi wamefanya Misri kupotoka" # wakuu wa Soani Soani ni mji kaskazini mwa Misri. # Nofu Huu ni mji katika sehemu ya kaskazini ya Misri. # wamefanya Misri ipotoke Neno "Misri" linawakilisha watu wa Misri. Kupotoka kunawakilisha kufanya kilicho kibaya. "kufanya watu wa Misri kupotoka" au "kufanya watu wa Misri kufanya kilicho kibaya" # Yahwe amechanganya roho ya upotoshaji miongoni mwake Isaya anazungumzia hukumu ya Yahwe kana kwamba Misri ilikuwa kikapu cha divai. Anazungumzia Yahwe kusababisha mawazo ya viongozi kupotoshwa kana kwamba mawazo yao yaliyopotoka yalikuwa kimiminiko ambacho Yahwe alichanganya kwa divai. "Yahwe amewahukumu kwa mawazo yao yaliyopotoka" au "Yahwe amewahukumu Misri kwa kupotosha mawazo ya viongozi wao, kama vinywaji vinavyolewesha huchanganya mawazo ya watu" # upotoshaji "upotovu" au "mchafuko" # miongoni mwake Hapa "mwake" ina maana ya Misri. Mataifa mara kwa mara huzungumziwa kana kwmaba ilikuwa wanawake. "ndani ya Misri" # wameiongoza Misri kupotea Hapa "wameiongoza" ina maana ya viongozi wanaoelezwa katika mistari iliyopita. Neno "Misri" inawakilisha watu wa Misri. "wakuu wamewaongoza watu wa Misri kupotoka" # wameiongoza Misri kupotea Kuongoza watu kupotoka inawakilisha kuwashawi kufanya kilicho kibaya. # kama mlevi anayepepesuka katika matapishi yake Isaya anazungumzia watu wa Misri kufanya kilicho kibaya kana kwamba walifanywa kuzurura kama mtu mlevi. # kama kichwa au mkia "Kichwa" ni sehemu ya mnyama au mtu anayopenda awe, inawakilisha kiongozi. "Mkia" ni kinyume na inawakilisha watu wanaofuata. "kama kiongozi au mfuasi" # tawi la mnazi au tete "tawi la mnazi" huota juu ya mti na linawakilisha watu ambao ni tajiri na muhimu. "Tete" huota katika maji mafupi na inawakilisha watu ambao ni maskini na wasio na umuhimu. "kama wao ni muhimu au sio muhimu" au "kama ni tajiri au maskini"