# Taarifa ya Jumla Hii inaendelea kulinganisha taifa la Israeli na shamba baada ya kuvunwa. # Masazo ya mavuno yatabaki Neno "masazo ya mavuno" hapa yanawakilisha watu ambao bado wanaishi Israeli. "Lakini kutakuwa na watu wachache waliosalia Israeli" # kama pale mzeituni unapotikiswa Watu walivuna mizeituni kwa kutikisa ili kwamba matunda yaweze kudondoka. "kama matunda machache ambayo yanabaki juu ya mizeituni baada ya watu kuivuna" # manne au matano Neno "matunda" linaeleweka kutoka kwa msemo kabla ya huu. "matunda manne au matano" # hili ni tamko la Yahwe Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tamko" ielezwe kama kitenzi "alitamka" au "alisema kwa dhati". "Hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati". # wanamume watamtazama kuelekea Muumba wao ... watamtazama Mtakatifu wa Israeli Kutazama kuelekea Mungu hapa inawakilisha kuwa na tumaini kuwa atawasaidia. "wanamume watakuwa na tumaini ya kwamba Muumba wao, Mtakatifu wa Israeli, atawasaidia" # wanamume watamtazama Neno "wanamume" linawakilisha watu kwa ujumla. "watu watamtazama" # macho yao yatatazama Hapa "macho" yanawakilisha watu ambao wanatazama. "watatazama" au"watu watatazama" # Mtakatifu wa Israeli Mtakatifu wa Israeli.