# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kumwambia Isaya anachotakiwa kufanya pale ambapo Yahwe atamtuma kuhubiri kwa watu. # Fanya mioyo ya watu hawa kutokuhisi Hapa "moyo" unawakilisha akili ya mtu. Mtu ambaye hafikiri kwa ufasaha na hawezi kuelewa na kujali juu ya kile kinachotokea inazungumziwa kana kwamba moyo wake hauna hisia. "Wafanye watu hawa kutoweza kuelewa" au "Fanya akili za watu hawa kufifia" # Fanya moyo wa watu hawa Inaweza kuwa kawaida zaidi kutafsiri "moyo" na "hawa" kama wingi. "Fanya mioyo ya watu hawa" # Fanya moyo ... kutokuhisi Amri hii ina maana ya kwamba Yahwe atatumia ujumbe wa Isaya kusababisha watu kuelewa kwa upungufu na kuwafanya kutojali kile Yahwe anachofanya. # masikio yao kufifia, na pofusha macho yao "fanya ya kwamba wasiweza kusikia, na fanya ya kwamba wasiweze kuona". Isaya kufanya watu kutoelewa ujumbe wa Yahwe au kile anachofanya kinazungumziwa kana kwamba Isaya alikuwa akiwafanya kuwa viziwi na vipofu. # waweze kuona kwa macho yao, kusikia kwa masikio yao Watu kuweza kuelewa ujumbe wa Yahwe na kile anachofanya inazungumziwa kana kwamba kama watu waliweza kuona na kusikia kimwili. # kuelewa kwa moyo wao Hapa "moyo" unawakilisha akili ya mtu. Kuelewa kwa ukweli jambo na kujali juu ya kile kinachoendelea inazungumziwa kana kwamba watu walipaswa kuelewa kwa mioyo yao. # kisha kugeuka Kutubu na kuanza kumtii Yahwe inazungumzwa kana kwamba watu waligeuka kwa Mungu kimwili. "mnifuate tena" au "kisha muanze kuniamini tena" # kuponywa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ningewaponya"