# Mtu atalazimishwa kuinama chini, na binadamu atashushwa Misemo inayotumika pamoja ina mana moja na inatumika pamoja kwa msisitizo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu atafanya kila mtu kuinama chini na kuwa wanyenyekevu". # Mtu atalazimishwa kuinama chini, na binadamu atashushwa Matukio ya siku za usoni yanazungumziwa kana kwamba vimekwisha tendeka. # Mtu atalazimishwa kuinama chini Kuinama chini mara kwa mara inaashria kuaibishwa. # macho ya mwenye majivuno yatakuwa chini Kuangalia chini mara nyingi ni ishara ya kuaibishwa. "macho ya watu wenye kiburi wataangalia chini kwa aibu" au "watu ambao wanamajivuno sasa wana aibu". # mwenye majivuno Hapa watu wenye kiburi, majivuno wanazungumziwa kana kwamba wapo juu zaidi ya watu wengine. "kiburi" # Yahwe wa majeshi atainuliwa katika haki yake Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu watamsifu Yahwe wa majeshi kwa sababu ni mwenye haki" # Yahwe wa majeshi Yahwe wa majeshi ya Israeli # atainuliwa Kuheshimiwa inazungumziwa kana kwamba ni kuinuliwa juu. "ataheshimiwa sana" # kondoo watakula kama kwenye malisho yao wenyewe Yahwe ataangamiza mji wa Yerusalemu, ambao uliitwa "shamba la mizabibu" katika 5:1. Litakuwa zuri bila chochote ila kwa ajili ya kondoo kula nyasi pale. # lisha kula nyasi # katika uharibifu, kondoo watalisha kama wageni Yaani, kondoo watalisha pale. Nchi itakuwa haina thamani kwa shughuli nyingine yoyote.