# Taarifa ya Jumla Katika fumbo hili, mmiliki wa shamba la mizabibu anaendelea kuzungumza juu ya shamba lake la mizabibu. # ondoa kitalu "ondoa mpaka wa vichaka". Kitalu ni safu ya vichaka au miti midogo ambayo ilipandwa ili kulinda bustani au eneo lingine lolote. Hapa "kitalu" huenda ina maana ya vichaka vya miiba ambavyo vilipandwa kuota katika ukuta wa mawe unaozunguka shamba la mizabibu. # nitaibadili kuwa malisho "nitaruhusu wanyama kwenda pale na kula". Hili ni eneo lenye nyasi ambapo wanyama hula. # itakanyagwa chini Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wanyama watapakanyaga chini" # nitailaza kuwa takataka "nitapaangamiza" # haitapogolewa wala kupaliliwa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu atapapunguza au kupapalilia" au "hakuna mtu atapakata matawi ambayo hayahitajiki, na hakuna mtu wa kutunza udongo" # mbigili na miiba itachipua juu Mbigili na miiba mara kwa mara hutumika kama alama za miji na nchi zilizoharibiwa.