# Taarifa ya Jumla Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. # Yuda na Yerusalemu "Yuda" na "Yerusalemu" ni mifano ya maneno kwa ajili ya watu wanaoishi pale. "wale wanaoishi katika Yuda na Yerusalemu" # katika siku za mwisho "katika siku za usoni" # mlima wa nyumba ya Yahwe utaimarishwa Hii inaweza kuwekwa 1) kama ufafanuzi. "Mlima wa nyumba ya Yahwe utasimama" au 2 katika hali ya kutenda. "Yahwe ataimarisha mlima ambapo hekalu lake linajengwa" # kama kilele cha milima Isaya anazungumzia umuhimu kana kamba ni urefu wa kihalisia. "sehemu muhimu zaidi ya milima" au "sehemu muhimu zaidi duniani" # itainuliwa juu zaidi ya vilima Isaya anazungumzia heshima kama sitiari kana kwamba ilikuwa urefu halisi. Hii inaweza kuwekwa 1) katika hali ya kutenda. "Yahwe atuheshimu kuliko kilima kingine" au 2) kama mfano wa maneno kwa ajili ya watu wanaoabudu pale. "Yahwe atawaheshimu watu ambao wanaabudu pale kuliko vile anavyoheshimu watu wengine wowote" # na mataifa yote Hapa "mataifa" ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu wa mataifa hayo. "na watu kutoka mataifa yote" # yatatiririka kwake Watu kuzunguka duniani kwenda katika mlima wa Yahwe inalinganishwa na jinsi mto unavyotiririka. Hii inasistiza ya kuwa watu wengi watakuja, sio tu watu wachache.