# Taarifa ya Jumla Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. # Miti ya mwaloni mitakatifu ... bustani Misemo hii ina maana ya sehemu ambapo watu wa Yuda waliabudu sanamu. # utaaibika kwa Baadhi ya tafsiri husema, "utaona aibu kwa sababu ya". Mtu huona aibu uso wake unapochemka, mara kwa mara kwa sababu anahisi amefanya kitu kibaya. # Kwa maana utakuwa kama mwaloni ambao majani hufifia, na kama bustani ambayo haina maji Maji hutoa uhai kwa miti na bustani. Watu wamejikata kutoka kwa Yahwe, ambaye hutoa uhai.