# Taarifa ya Jumla Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. # hapo mwanzo ... hapo mwanzo Hizi ni njia mbili za kuzungumzia sehemu ya kwanza au mwanzo wa historia ya Israeli, pale ambapo Israeli ilipokuwa taifa. # utaitwa Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "watu watakuita" # mji wa utakatifu, mji mwaminifu Hapa "mji" una maana ya watu wanaoishi Yerusalemu. "mji ambao watu ni watakatifu na waaminifu kwa Mungu"