# Taarifa ya Jumla Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. # Taifa, wenye dhambi Maana zawezekana kuwa 1) Isaya anasema mambo mawili tofauti juu yao. "Taifa la Israeli, nyie wenye dhambi" au 2) anasema jambo moja tu kuhusu wao. "Taifa la wenye dhambi" # watu waliolemewa kwa udhalimu Kitu kizito sana ambacho mtu anweza kubeba ni sitiari ya dhambi nyingi. "dhambi yao ni kama mfuko mzito juu ya mabega yao unaowafanya vigumu kwao kutembea" # mtoto wa waovu Neno "mtoto" ni sitiari ya watu ambao hufanya kile wengine walichokwisha fanya. "watu ambao hufanya uovu ule ule wanaouona wengine wakifanya" # tenda mabaya fanya mambo maovu # Wamemtelekeza Yahwe "Wameondoka mbali kutoka kwa Yahwe" # wamemdharau "wamekataa kutii" au "wamekataa kuheshimu" # Israel Yuda ni sehemu ya iliyokuwa taifa la Israeli. # Wamejitenganisha kutoka kwake Ingawa katika kipindi kimoja walikuwa marafiki, kwa sasa wanamtendea kana kwamba hawamjui.