# Taarifa ya Jumla Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. # Sikieni, enyi mbingu, na sikilizeni, enyi nchi Ingawa unabii huu ulikusudiwa kwa ajili ya watu wa Yerusalemu na Yuda kusikiliza, Isaya anafahamu hawatasikiliza. Maana zawezekana kuwa 1) anazungumza kwa kifupisho, kana kwamba "mbingu" na "nchi" zingeweza kusikiliza kile Yahwe alichosema, au 2) maneno "mbingu" na "nchi" ni mifano ya maneno na neno la ujumla kwa ajili ya viumbe vyote hai kila sehemu. "wewe ambaye unaishi katika mbingu ... wewe ambaye unaishi juu ya nchi" # Yahwe Hili ni jina la Mungu ambalo alilifunua kwa watu wake katika Agano la Kale. # Nimewarutubisha ... haielewi Maneno ambayo Yahwe alizungumza na ambayo Isaya anazungumza kwa Waisraeli kwa niaba ya Yahwe. # Nimewarutubisha na kuwakuza watoto Yahwe anazungumza kana kwamba maneno yake yalikuwa chakula na kana kwamba Waisraeli walikuwa watoto wake. "Nimewatunza watu wanaoishi Yuda kama walikuwa watoto wangu" # punda kihori cha kulisha cha bwana wake Unaweza kuiweka wazi taarifa inayoeleweka. "punda anajua kihori cha kulisha cha bwana wake" au "punda anajua ni wapi bwana wake humpatia chakula" # lakini Israeli haijui, Israeli haielewi Yawezekana hii ina maana ya "lakini watu wa Israeli hawanijui, hawaelewi ya kuwa mimi ndiye ninayewatunza" # Israeli Huu ni mfano wa maneno kwa ajili ya watu wa Israeli. Yuda ni sehemu ambayo ilikuwa taifa la Israeli. "watu wa Israeli"