# Taarifa ya jumla: Bwana anazungumza. # Watu wanaoishi katika kivuli chake watarejea Watu wa Israeli tena wataishi kwa kulindwa na Mungu. # watafufuliwa kama nafaka na maua kama mizabibu Mafanikio ya Israeli yanazungumzwa kwa lugha ya kilimo. # Utukufu wake utakuwa kama divai ya Lebanoni Kama divai ya Lebanoni ilivyokuwa maarufu pia Israeli itakuwa maarufu. # nifanye nini tena na sanamu? Sentensi hii inaonesha kuwa Mungu atawakataza Israeli kuabudu muingu. # kama mberoshi majani yake ni ya kijani daima Mberoshi ni mti ambao majani yake ni ya kijani mwaka mzima. Hii inawakilisha baraka za Bwana juu ya Israeli. # kwangu huja matunda yako "matunda" inawakilisha kitu kizuri kinachotoka kwa Bwana.