# Taarifa ya jumla: Bwana anazungumza. # ifanyieni haki, vuneni matunda ya uaminifu wa agano Haki na agano vimezungumzwa kama mazao ambayo yanapandwa na kuvunwa. # Chimbueni ardhi yenu isiyopandwa Ardi isiyolimwa haipo tayari kwa kupandwa. Bwana anataka watu watubu ili waanze kufanya mambo yanayofaa. # Mmelima uovu; mmevuna udhalimu. Uovu na udhalimu vimezungumzwa kama mazao ambayo yanapandwa na kuvunwa. # Mmekula matunda ya udanganyifu Matokeo ya udanganyifu yanazungumzwa kama chakula ambacho kinaweza kulika.