# Taarifa ya jumla: Mungu anazungumza juu ya Yuda na Israeli. # Kwa hiyo nitakuwa kama simba kwa Efraimu Bwana ataenda kuishambulia Efraimu kama simba. # kama mwana simba kwa nyumba ya Yuda Bwana atawatendea Yuda vivyo hivyo. # Mimi, naam mimi Bwana anasisitiza kuwa yeye ataleta hukumu kwa watu wake wote. # Nitararua Kama simba anavyorarua mnyama anayemla hivyo Bwana atawararua watu waketoka kwenye nyumba na nchi yao. # Nitakwenda na kurudi mahali pangu Bwana atawaacha waasi. # na kutafuta uso wangu Kujaribu kwenda katika uwepo wa Mungu kwa njia ya kuabudu na kafara.