# Taarifa ya jumla: Mungu anazungumza juu ya Yuda na Israeli. # nitakuwa kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa nyumba ya Yuda Bwana ataangamiza mataifa yote. # Nondo ... uozo Maneno haya yanatafsiriwa kwa njia mbali mbali kwa sababu maana ya kiebrania ni pana sana na isiyo na uhakika. # Efraimu alipoona ugonjwa wake, Yuda akaona jeraha lake Efraimu na Yuda wote walitambua kuwa wapo kwenye hatari. # Efraimu akaenda Ashuru; Yuda akatuma wajumbe kwa mfalme mkuu Efraimu na Yuda walimuomba Ashuru msaada badala ya kumuomba Mungu awasaidie. # Lakini hakuweza Hapa anazungumziwa mfalme wa Ashuru.