# Taarifa ya jumla: Mungu anazungumza juu ya Israeli. # Piga tarumbeta huko Gibea, na tarumbeta huko Rama. Amri inatolewa kwa watu wa Gibea na Rama kusistiza kuwa adui anakuja. # Sauti ya kilio cha vita huko Beth Aveni 'Tutakufuata, Benyamini!' Hili ni ombi kuwa askari wa Benyamini wawaongoze watu katika vita. # Beth Aveni Huu ni mji uliokuwepo mpakani kati ya ufalme wa kaskazini mwa Israeli na kabila la Benyamini kusini mwa ufalme. # Miongoni mwa makabila ya Israeli nimetangaza habari itakayotokea. "Nitafanya katika kabila la Israeli yale niliyosema"