# Taarifa ya jumla: Bwana anazungumza kuhusu Israeli. # Najua Efraimu, na Israeli hajajificha kwangu "Efraimu" na "Israeli" ni watu ambao wanaishi kaskazini mwa ufalme wa Israeli. Hapa Mungu anasema kuwa anawafahamu wao ni akina nani na nini wanafanya. # Efraimu, sasa umekuwa kama kahaba Efraimu amesimama kama kahaba kwa sababu watu sio waaminifu kwa Mungu kama vile kahaba sio mwaminifu kwa mwanaume mmoja. # maana mawazo ya uzinzi yako ndani yao Hii inamaanisha kuwa wanatamani kutokuwa waaminifu kwa Mungu. Wanataka kuabudu miungu. # kumgeukia Mungu ... hawatamjua Bwana. "kunigeukia mimi ... hawakunijua mimi" au "kunigeukia mimi ... hawakunijua mimi, Bwana." # na hawatamjua Bwana Israeli hawakumtii tena Mungu kwa namna yoyote. Hawakumtambua Bwana kama Mungu wao.