# Taarifa ya jumla Bwana anazungumza na Hosea. # Mashtaka Haya ni malalamiko ya mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine mahakamani. # Mama yako Hapa "mama" inamaanisha taifa la Israeli. # kwa kuwa yeye si mke wangu Bwana anaeleza kuwa Israeli inazungumzwa kama mwanamke ambaye hatendi kama mke kwa Bwana. Badala yake Israeli amegeuka na kuacha kumfuata na kumwabudu yeye. # wala mimi si mumewe Bwana hawezi kuendelea kuwa na uhusiano na taifa la Israeli kama mume kwa mke wake. # na matendo yake ya uzinzi Mke ambaye ni mzinzi anamuacha mume wake na kulala na mwanaume mwingine. Hivi ndivyo Israeli alivyofanya mbele ya Bwana. # kati ya matiti yake Israeli wanategemea miungu na sio Bwana. # nitamvua nguo na kumuonyesha uchi wake kama siku aliyozaliwa Bwana hataendelea kuwalinda na kuwasaidia Israeli kwa sababu taifa limemwacha. # nitamfanya kama jangwa Bwana ataibadilisha Israeli ifanane na jangwa ambao nii mji usiozalisha. # nitamfanya afe kutokana na kiu Hapa "kiu" inamaana ya uhitaji wa kumwabudu Bwana na sio miungu mingine, au Israeli hawatatweza kuishi kama taifa.