# Sasa Hii inaonyesha sehemu mpya ya barua. Hapa mwandishi anatoa maoni yake ya mwisho kwa wale anaowaandikia. # ndugu Hii inamaanisha waumini wote anaowandikia wanume au wanawake. # huchukuliana na neno la kutia moyo "kwa uvumilivu fikirini juu ya nilichokiandika kuwatieni moyo. # neno la faraja "Neno" hapa linasimama kwa niaba ya ujumbe. # amewekwa huru "hayuko tena gerezani"