# Maelezo ya Jumla: Abeli alikuwa mwana wa mwanamme na mwanamke wa kwanza, Adamu na Eva. Pia Kaini mwana wao alimuua Habili. # Mlima Sayuni Mwandishi anaongea Mlima Sayuni, hekalu la mlima Yerusalem kana kwamba lenyewe ilikuwa mbingu, nyumbani kwa Mungu. # Wamekuja Wamewasili # Malaika elfu kumi "Idadi isiyohesabika ya malaika" # mzaliwa wa kwanza Hii inaongea waumini katika Kristo kana kwamba ni wana ambao ni wazaliwa wa kwanza. Hii inasisitiza sehemu yao maalumu na faida kama watu wa Mungu. # mmesajiliwa mbinguni "ambao majina yao yameandikwa mbinguni # mpatanishi wa agano jipya Hii inamaana Yesu alisababisha agano jipya kuwepo kati ya Mungu na wanadamu # Mmekamilishwa "ambao Mungu amewafanya wakamilifu" # Damu ya kunyunyiza ambayo hunena zaidi kuliko damu ya Habili. "Damu ya Yesu iliyonyunyizwa ambayo inamaana kubwa zaidi kuliko damu ya Habili, ambaye aliuawa na Kaini" # damu damu hapa inasimama kwa kifo cha Yesu, kama damu ya Habili inavyoisimama kwa kifo chake.