# baba katika mwili Neno "mwili" hapa linamaanisha mwanadamu. # kama warudiaji/ wanaotunidhamisha wanao turudi # Je hatupaswi hata zaidi kumtii Baba wa kiroho na kuishi? Mwandishi anatumia swali kusisitiza kwamba wangeweza kumtii Mungu Baba, # na ishi "ili kwamba tuishi" # Baba wa roho "Baba yetu wa kiroho" au Baba yetu wa mbinguni" # ili tushiriki utakatifu wake "ili kwamba tuwe watakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu" # tunda la amani "Tunda" hapa ni alama na inaongelewa kana kwamba ni mtu aliye katika amani na ambaye alileta amani kwa wengine. # tunda la utauwa Utauwa, ni hali ya mtu anaye mtii Mungu, inaongelewa kana kwamba ni tunda linakuwa juu ya mti. Mwandishi hapa anasema kwamba utauwa unaongezeka kama matokeo ya kurudiwa. # wale waliofundishwa nayo "wale walio fundishwa kwa kurudiwa." Ambao Mungu amewafundisha kwa kuwarudi."