# Maelezo ya Jumla: Hii inaendeleza nukuu ya nabii Yeremia katika Agano la Kale # Sitazikumbuka dhambi zao na makosa yao Hii ni sehemu ya pili ya ushuhuda wa Roho Mtakatifu (tazama 10:15). Kisha asema, "Sitazikumbuka dhambi zao na makosa yao." # Sitazikumbuka dhambi zao "Sitazikumbuka dhambi zao"au "sitafikiri tena kuhusu dhambi zao" # Sasa Hii haimaanishi "wakati huu," lakini imetumika kuvuta usikivu kwa kipengele kinachofuata. # mahali palipo na msamaha kwa mambo haya "wakati Mungu aliposamehe mambo haya" # hakuna tena dhabihu yeyote kwa ajili ya dhambi "watu wao hawahitajiki kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi"