# Sentensi Unganishi: Mwandishi anasisitiza kwamba Kristo (sasa yuko mbinguni anatuombea) alipaswa kufa mara moja tu kwa ajili ya dhambi na kwamba atarudi duniani mara ya pili. # nakala ya vitu vya mbinguni vinapaswa kusafishwa kwa dhabihu ya hawa wanyama "Makuhani wanapaswa kutumia dhabihu hii ya wanyama kusafisha nakala za vitu vya mbinguni" # vitu vya mbinguni vyenyewe vilipaswa visafishwe kwa dhabihu zilizo bora zaidi Ile ni bora zaidi ya dahabihu zilizotumika kusafisha nakala za duniani. Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "kama kwa vitu vya mbinguni vyenyewe, Mungu alipaswa kuvisafisha kwa dhabihu iliyo bora" # ilitengenezwa kwa mikono "Mikono" hapa inamaanisha mwanadamu. AT: "ambayo wanadamu walitengeneza na" # ya kitu halisi "sehemu ya kweli na takatifu ya patakatifu pa patakatifu"