# kunyunyiziwa kwa majivu kwa hao ambao hawajatakaswa Kuhani angemimina kiasi kidogo cha majivu kwa watu wasiosafi. # je si sana zaidi damu ya Yesu...kuosha nafsi zetu kutoka katika matendo mafu ili kumtumikia Mungu aliye hai? Mwandishi anatumia nukuu kusisitiza kwamba dhabihu ya Kristo ilikuwa na nguvu. AT: Hivyo hakika damu ya Kristo itatusafisha nafsi zetu hata zaidi kutoka katika kazi/ matendo mafu na kumtumikia Mungu aliye hai! Kwa sababu, kupitia kwa kupitia Roho wa milele, alijitoa mwenyewe pasipo hatia kwa Mungu. # damu ya Kristo "damu" ya Yesu inasimama kwa kifo chake. # kusafisha dhamiri zetu "Dhamiri" hapa inamaanisha mtu kujisikia hatia. Kwa sababu Yesu alijidhabihu yeye mwenyewe, waumini hawapaswi tena kujisikia hatia kwa ajili ya dhambi zao walizozifanya kwa sababu amewasamehe. # waa Hii ni dhambi ndogo au kosa la kimaadili hapa linaongelewa kana kwamba lilikuwa dogo,doa lisilo la kawaida kuharibu juu ya mwili wa Kristo. # safisha "kusafisha" linasimama kwa tendo la nafsi zetu kupokea msamaha wa kutokuwa na hatia kwa ajili ya dhambi tulizozitenda # hao walioitwa na Mungu wale ambao Mungu amewateua au kuchaguliwa na kuwa watoto wake # Kazi/ matendo mafu matendo mafu yanaongelewa kana kwamba yalikuwa yakitoka katika ulimwengu wa wafu. # Kwa sababu hii "kama matokeo" au "kwa sababu hii" # Ni mjumbe/ mpatanishi wa agano jipya Hii inamaanisha Kristo alisababisha agano jipya kati ya Mungu na wanadamu kuwepo. # agano la kwanza tafsiri hii kama ulivyotafsiri 8:6 # wale walioitwa Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. AT: "wale ambao Mungu aliowachagua kuwa wana wake" # urithi upokeaji wa kile ambacho Mungu alikuwa amewaahidi waumini kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kurithi kitu na mali kutoka katika mwanafamilia.