# Maelezo ya Jumla: Hii inaendeleza nukuu kutoka kwa nabii Yeremia. # Hawatafundishana kila mmoja na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, akisema, 'Mjue Bwana.' Nukuu hii ya moja kwa moja inaweza kuengelewa kana kwamba ni nukuu isiyo ya moja kwa moja. AT: "Hawatahitaji kuwafundisha jirani zao au ndugu za kunijua" # jirani... ndugu Haya maneno mawili yanalenga Waisraeli wenzao. # Kumjua Bwana...wote watanijua mimi Neno "kujua" hapa linasimama kwa maana ya kutambua. # kwa matendo yao yasiyo ya haki Hili linasimama kwa ajili ya watu waliofanya matendo haya yasiyo ya haki. # Sitazikumbuka dhambi zao tena Neno "kumbuka" linamaanisha "sitafikiri kuhusu dhambi hizo"