# Maelezo ya Jumla: Nukuu hii inatoka kwa nabii Yeremia. # nyumba ya Israeli Watu wa Israeli wanaongelewa kana kwamba walikuwa ni nyumba. # baada ya siku hizo "baada ya wakati huo" # nitaweka sheria zangu mioyoni mwao Sheria za Mungu zinaongelewa kana kwamba ni vyombo ambavyo vingeweza kuwekwa mahali fulani. Uwezo wa watu kufikiri kunaongelewa kana kwamba ni sehemu.AT: "Nitawawezesha kuelewa sheria zangu" # Pia nitaziandika mioyoni mwao Mioyo ya watu ilifikiriwa kuwa kituo cha uaminifu kwa Mungu, na imeongelewa kana kwamba ni ukurasa ambao ungeweza kuandikwa. # nitakuwa Mungu wao "Nitakuwa Mungu wanae mwabudu" # watakuwa watu wangu "watakuwa watu ambao ninawajali"