# Sentensi Unganishi: Sehemu hii inaanza kwa kuonyesha kwamba agano jipya ni bora kuliko agano la kale la Israeli na Yuda. # Kristo amepokea "Mungu amempa Kristo" # huduma iliyo bora zaidi. kama alivyo mpatanishi wa agano bora "huduma iliyo bora zaidi, kama Kristo alivyo mpatanishi wa agano bora" # mpatanishi wa agano bora Hii ina maanisha kuwa Kristo alisababisha agano bora kuendelea kati ya Mungu na wanadamu. # ambalo liko katika ahadi bora Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: ''ni agano hili ambalo Mungu alilifanya kulingana na ahadi zilizo bora" au "Mungu aliahidi vitu bora wakati alipofanya agano hili" # Aagano la kwanza... agano la pili Haya maneno "kwanza" na "pili" ni namba za kawaida. AT:" agano la zamani ... agano jipya" # halingekuwa na makosa "ingekuwa kamilifu"