# ardhi iliyopokea mvua inyeshayo mara kwa mara juu yake ardhi inufaikayo na mvua nyingi inaongelewa kana kwamba ni mtu aliyekunywa maji mengi ya mvua. # ikatoa mazao muhimu Ardhi izaayo mazao inaongelewa kana kwamba iliwazalia. # kwa hao waliofanya kazi katika ardhi Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "kwa wale kwa ajili yao mtu aliandaa ardhi" # ardhi hupokea baraka kutoka kwa Mungu Mvua naa mazao vinaonekana kama ushahidi kama Mungu amemsaidia mkulima. Ardhi inaongelewa kana kwamba ni mtu ambaye angeweza kupokea baraka za Mungu. # ipo katika hatari ya kulaaniwa Hii inaongelea "laana" kana kwamba ni ilikuwa ni sehemu ambayo mtu angeweza kukaribia. AT: "iko katika hatari ya Mungu kuilaani. # Mwisho wake ni kuteketezwa Mungu atasababisha kila kitu katika shamba hilo kuteketea.