# aliyeziingia mbingu "aliyeingia mahali alipo Mungu" # Mwana wa Mungu Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu. # tushikilie sana imani zetu imani na tumaini vinaongelewa kana kwamba ni vitu ambavyo mtu angeweza kuvikumbatia. # hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kutuhurumia... Badala, tunaye Maneno haya yakukanusha yanalenga kuonyesha kwamba Yesu ni mwenye huruma kwa watu . AT: " tunaye kuhani mkuu anayeweza kutuhurumia...Kweli tunaye" # kiti cha enzi cha neema "kiti cha enzi cha Mungu, pale palipo na neema" au "pale Mungu, ambaye ni neema, ameketi katika kiti chake cha enzi" # yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi Hii inaweza kusemwa katikamfumo tendaji. AT: "yeye ambaye amevumilia majaribu katika kila hali tunayoipitia" au "ambaye movu amekuwa akimjaribu katika kila njia anavyotujaribu" # hana dhambi "hakutenda dhambi" # kiti cha enzi cha neema "kwemye kiti cha enzi cha Mungu palipo na neema." "kiti cha enzi" hapa kina maanisha utawala wa Mungu kama mfalme. # ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji. "rehema" na "neema" hapa vinaongelewa kana kwamba ni vitu ambavyo vinaweza kupewa au kupatikana.