# bado imewekwa kwa baadhi kuingia katika pumziko Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu vinaongelwa kana kwamba zilikuwa pumziko la kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda. Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji.AT: "Mungu bado anaruhusu baadhi ya watu kuingia katika sehemu yake ya pumziko. # kama mtasikia sauti yake Amri za Mungu kwa Waisraeli zinaongelewa kana kwamba alikuwa amewapa kwa sauti. AT: "kama mtasikia Mungu akiongea" # msifanye mioyo yenu kuwa migumu kutosikia kunaongelewa kana kwamba ni moyo ulikuwa umwefanya kuwa mgumu. AT: "Msiwe wenye mioyo migumu." Tafsiri kama ulivyofanya 3:7.