# Maelezo ya Jumla: Nukuu ya kwanza hapa (Kama nilivyoapa...) inatoka katika Zaburi, na nukuu ya pili (Mungu akapumzika...) inatoka katika Maandiko ya Musa, na ya tatu (Hawataingia...) inatoka katika Zaburi. # Sisi tulioamini "sisi tulioamini" # watakao ingia katika pumziko hilo Amani na ulinzi alioutoa Mungu vinaongelewa kana kwamba vilikuwa ni pumziko ambazo anaweza kuwapa, na kana kwamba ilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeenda. # Kama alivyo sema "Kama vile Mungu alivyosema" # Kama nilivyo apa katika hasira yangu "Kama nilivyo apa wakati nilipokuwa nimekasirika sana" # Hawataingia kwenye pumziko langu Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu vinaongelwa kana kwamba zilikuwa pumziko la kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda. # kazi yake ya uumbaji ilimalizika Hii inaweza kuwekwa katika mfumo tendaji. AT: "alimaliza uumbaji" au "alimaliza kazi zake za uumbaji" # tangu mwanzo wa dunia/ ulimwengu Mwandishi anaongelea dunia kana kwamba ni jengo lililowekwa kwenye kwenye msingi. # siku ya saba Hii inasimama kama badala ya "saba"