# Maelezo ya Jumla Nukuu hii inatoka katika Zaburi nyingine. # Lakini ni malaika gani wakati wowote Mungu amesema...miguu? Mwandishi anatumia swali kusisitiza kwamba Mungu hajawahi kumwambia malaika. AT: '"Lakini Mungu hajamwambia malaika yeeyote wakati wowote"' # Keti mkono wangu wa kulia Hapa mkono wa kulia unamaanisha sehemu ya heshima. AT: "Kaa karibu yangu katika sehemu ya heshima" # Hadi nitakapo waweka maadui wako chini ya miguu yako Maadui wa Kristo wanaongelewa kana kwamba watakuwa chombo ambachomfalme anaweka miguu yake, Picha hii inawakilisha kushindwa na aibu kwa maadui wake. # Sio malaika wote ni roho... wanarithi wokovu Mwandishi anatumia hili swali kuwakumbusah wasomaji wake kwamba malaika hawana nguvu kama Kristo, lakini wana jukumu tofauti. AT: "malakia wote ni roho ambazo... hurithi wokovu." # kwa wale watakaorithi wokovu Kupokea kile ambacho Mungu amewaahidi waumini imeongelewa kana kwamba wanarithi utajiri na mali kutoka katika mwana familia. AT: "kwa ajili ya wale wote ambao Mungu atawaokoa"