# kuinamisha nyuso zao mbele zake Walilala chini kifudifudi kuelekea ardhini. Hii ni ishara ya unyenyekevu na heshima kwa Yusufu. # Je mimi ni badala ya Mungu? Yusufu anatumia swali kuwatia moyo ndugu zake. "Mimi sipo katika nafasi ya Mungu" au "Mimi sio Mungu" # mlikusudia kunidhuru "mlikusudia kutenda uovu dhidi yangu" # Mungu alikusudia mema "Mungu alikusudia kwa wema" # Hivyo basi msiogope "Kwa hiyo msiniogope" # Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo "Nitahakikisha nyie pamoja na watoto wenu mnapata chakula cha kutosha" # aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole. "Aliwatia moyo kwa kuzungumza nao kwa upole"