# Maelezo ya Jumla: Yakobo anaendelea kuzungumza na wanawe. # lililomo lilinunuliwa Ununuzi unaweza kuwekwa wazi. "ndani mwake ulinunuliwa na Abrahamu" # kutoka kwa watu wa Hethi "kutoka kwa Wahiti" # alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe "alimaliza kuwaagiza wanawe" au "alimaliza kuwaamuru wanawe" # akaiweka miguu yake kitandani Yakobo alikuwa amekaa juu ya kitanda. Sasa, Yakobo anageuka na kuweka miguu yake kitandani ili aweze kulala chini. # akavuta pumzi ya mwisho Hii ni njia ya upole ya kusema mtu amekufa. # akawaendea watu wake Baada ya Yakobo kufa, nafsi yake ilikwenda sehemu ile ile kama ndugu zake waliokufa kabla yake.