# Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli "Haya" ina maana ya wana wa Yakobo waliotajwa katika 49:1-27. Kila mwana alikuwa kiongozi wa kabila lake mwenyewe. # alipowabariki Hapa neno "alipowabariki" lina maana ya kuongelea baraka rasmi. # kila mmoja kwa baraka iliyomstahili "Akawapa kila mtoto baraka inayomstahili" # akawaelekeza "akawaamuru" # Ninakaribia kwenda kwa watu wangu Hii ni njia ya upole ya kusema ya kwamba amekaribia kufa. "Nimekaribia kufa" # kwenda kwa watu wangu Yakobo ana maanisha pale ambapo nafsi yake utakwenda atakapokufa. Anategemea kuwaunga Abrahamu na Isaka katika maisha ya baadae. # Efroni Mhiti Hili ni jina la mwanamume. "Mhiti" ina maana ya "uzao wa Hethi". # Makpela Makpela lilikuwa jina la eneo au mahali. # Mamre Hili lilikuwa jina lingine la mji wa Hebroni. Inawezekana lilitajwa baada ya Mamre, rafiki wa Abrahamu aliyeishi kule.