# Dani atawaamua watu wake Hapa "Dani" ina maana ya uzao wake. "Uzao wa Dani utawaamua watu wake" # watu wake Maana zinazowezekana za "watu wake" ni 1) "watu wa Dani" au 2) "watu wa Israeli" # Dani atakuwa nyoka kando ya njia Yakobo anazungumza kuhusu Dani na uzao wake kana kwamba walikuwa nyoka. Ingawa nyoka ni mdogo, inaweza kumshusha aongozaye farasi chini ya farasi wake. Kwa hiyo Dani, ingawa kabila dogo, ni la kutisha sana kwa adui zake. "Uzao wa Dani utakuwa kama nyoka kando ya barabara" # Ninaungoja wokovu wako, Yahwe. Nomino inayojitegemea "wokovu" inaweza kutafsiriwa kama "kuokoa". "Ninakusubiri, Yahwe, kunikoa" # Ninaungoja Neno "Ninaungoja" ina maana ya Yakobo.