# Yuda ni mwana simba Yakobo anamzungumzia Yuda kana kwamba alikuwa mtoto wa simba. Yakobo anasisitiza nguvu ya Yuda. "Yuda ni kama mwana wa simba" # Mwanangu, umetoka katika mawindo yako "Wewe, mwanangu, umerudi kutoka kula windo lako" # kama simba jike Yakobo anamlinganisha Yuda na simba jike. Simba jike ni mwindaji na mlinzi wa msingi wa watoto wake. # Je nani atakayejaribu kumwamsha? Yakobo anatumia swali kusisitiza jinsi Yuda anavyotisha watu wengine. "Hakuna atakaye kumuamsha"