# kuuona uso wako tena Hapa "uso" ina maana ya mtu mzima. "Kukuona mara nyingine" # katikati ya magoti ya Israeli Yusufu alipowaweka wanawe juu ya mapaja ya Israeli au magotini ilikuwa ishara ya kwamba Israeli alikuwa akiwachukua. Hii iliwapa watoto hawa urithi maalumu kutoka kwa Yakobo. # kisha akainama na uso wake juu ya nchi Yusufu aliinama chini kuonyesha heshima kwa baba yake. # Manase katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kulia wa Israeli Yusufu anawaweka wavulana ili kwamba Israeli aweze kuweka mkono wake wa kuume juu ya Manase. Manase alikuwa ndugu mkubwa na mkono wa kulia ilikuwa ishara ya kwamba angepokea baraka kubwa.