# Wakamwambia "Wakamwambia Yakobo" # maneno yote ya Yusufu aliyokuwa amewaambia Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. "kila kitu ambacho Yusufu alikisema kwao" # roho ya Yakobo baba yao ikafufuka Neno la "roho" lina maana ya mtu mzima. "Yakobo baba yao alipona" au "Yakobo baba yao akawa na furaha sana"