# kuwahifadhi kama masalia duniani "ili kwamba wewe na familia yenu msipotee kutoka duniani" au "kuhakikisha vizazi vyako vinaendelea kuishi" # kuwaweka hai kwa ukombozi mkuu Nomino inayojitegemea "ukombozi" inaweza kuwekwa kama "kuokoa". "kukuweka hai kwa kuwaokoa kwa njia ya juu" # amenifanya baba kwa Farao Yusufu kumshauri na kumsaidia Farao inazungumziwa kana kwamba Yusufu alikuwa baba wa Farao. "amenifanya niwe kiongozi kwa Farao" au "amenifanya kuwa mshauri mkuu kwa Farao" # nyumba yake yote Hapa "nyumba" ina maana ya watu wanaoishi ndani ya kasri yake. "miongoni mwa nyumba yake yote" au "kati ya wote wa kasri yake" # mtawala wa nchi yote ya Misri Hapa "nchi" ina maana ya watu. "mtawala juu ya watu wote wa Misri" # mtawala Hapa Yusufu anamanisha ya kwamba yeye ni mtawala katika nafasi ya pili kutoka kwa Farao, mfalme wa Misri. Taarifa hii inayoeleweka inaweza kuwekwa wazi.