# Tutainuka na kwenda ili kwamba tuishi tusife, wote sisi, wewe, na hata watoto wetu Misemo hii "ili kwamba tuishi" pamoja na "tusife" ina maana moja. Yuda anaweka msisitizo ya kwamba wanalazimu kununua chakula Misri ili kwamba waishi. "Tutakwenda Misri na kupata nafaka ili familia yetu yote iweze kuishi" # Tutainuka Hapa "tutainuka" ina maana ya ndugu ambao watasafiri kwenda Misri. # ili kwamba tuishi Hapa "tuishi" ina maana ya ndugu, Israeli na familia nzima. # wote sisi Hapa "sisi" ina maana ya hawa ndugu. # sisi, wewe Hapa "wewe" ni umoja na ina maana ya Israeli. # na hata watoto wetu Hapa "wetu" ina maana ya hawa ndugu. Hii ina maana ya watoto wadogo ambao wangeweza kufa katika kipindi cha njaa. # Mimi nitakuwa mdhamini wake Nomino inayojitegemea "mdhamini" inaweza kuwekwa kama kitenzi "ahidi". "Ninaahidi kumrudisha" # Utaniwajibisha mimi Jinsi ambavyo Yakobo atamuwajibisha Yuda inaweza kuwekwa wazi. "Utanifanya niwajibike kwako kuhusu kitakachotokea kwa Benyamini" # basi nibebe lawama Hii inazungumzia kuhusu "lawama" kana kwamba ilikuwa kitu ambacho mtu anaweza kubeba. "Unaweza kunilaumu" # Kwani kama tusingekawia Yuda anaelezea jambo ambalo lingetokea hapo nyuma lakini halikutokea. Yuda anamkaripia baba yake kwa kusubiri muda mrefu sana kuwatuma wanawe Misri kufuata chakula zaidi. # tungekuwa tumekwisha rudi mara ya pili "tungekuwa tumerudi mara mbili"