# Njaa ilikuwa kali katika nchi Neno "Kaanani" linaeleweka. Taarifa hii inaweza kuwekwa wazi. "Njaa ilikuwa kali katika nchi ya Kaanani" # Ikawa Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. # walipokuwa wametumia chakula "Yakobo na familia yake walipokuwa wamekula" # walichokitoa "wana wakubwa wa Yakobo walileta" # mtununulie Hapa "mtununulie" ina maana ya Yakobo, wanawe, na familia yake iliyobaki.