# Katika siku ya tatu Neno "tatu" ni mpangilio wa namba."baada ya siku ya pili" # Fanyeni hivi nanyi mtaishi Taarifa inayotambulika inaweza kuwekwa wazi. "Kama utafanya kile nilichosema, nitakuruhusu uishi" # ninamcha Mungu Hii ina maana ya kumheshimu Mungu kwa dhati na kuonyesha heshima hiyo kwa kumtii yeye. # mmoja wenu atazuiliwa hapa gerezani Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "muache mmoja wa ndugu zako hapa gerezani" # lakini ninyi nendeni Hapa "ninyi" ni wingi na ina maana ya ndugu wote ambao hawatakaa gerezani. "lakini ninyi mliosalia" # chukueni nafaka kwa ajili ya nyumba zenu Hapa "nyumba" ina maana ya familia. "beba nafaka hadi nyumbani kusaidia familia zenu wakati wa njaa hii" # ili kwamba maneno yenu yathibitishwe Hapa "maneno" yana maana ya kile kilichosemwa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ili niweze kujua kile mnachosema ni kweli" # nanyi hamtakufa Hii inaashiria ya kwamba Yusufu angewafanya maaskari wake kuwaua ndugu iwapo angetambua ya kwamba walikuwa wapelelezi.