# Ninyi ni wapelelezi Wapelelezi ni watu ambao kwa siri hujaribu kupata taarifa kuhusu nchi ili kuisaidia nchi nyingine. # Mmekuja kuona sehemu za nchi Maana kamili inaweza kuwekwa wazi. "Mmekuja kujua ni wapi hatulindi nchi yetu ili kwamba muweze kutushambulia" # bwana wangu Hii ni njia ya kuonyesha heshima kwa mtu. # Watumishi wako wamekuja Ndugu hawa wanajitambulisha kama "watumishi". Hii ni njia maalumu ya kuongea na mtu mwenye mamlaka makubwa zaidi. "Sisi, watumishi wako, tumekuja" au "Tumekuja"