# Yusufu akawaona ndugu zake na kuwatambua "Yusufu alipowaona ndugu zake, aliwatambua" # alijibadili kwao "alijifanya kana kwamba hakuwa kaka yao" au "hakuwafahamisha ya kwamba alikuwa kaka yao" # Mmetoka wapi? Hili halikuwa swali la balagha ingawa Yusufu alijua jibu. Ilikuwa sehemu ya maamuzi yake kuficha utambulisho wake kwa ndugu zake.