# Basi Yakobo akafahamu Neno "basi" inaweka alama ya sehemu mpya ya simulizi. # Kwa nini mnatazamana? Yakobo anatumia swali kukaripia watoto wake kwa kutofanya kitu chochote kuhusu nafaka. "Msikae hapo tu!" # Shukeni huko ... chini Ilikuwa kawaida kuzungumza kuhusu kwenda kutoka Kaanani mpaka Misri kama kwenda "chini" # kutoka Misri Hapa "Misri" ina maana ya watu kuuza nafaka. "kutoka kwa wale wauzao nafaka ndani ya Misri" # Benjamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumtuma Benyamini na Yusufu walikuwa na baba mmoja na mama. Yakobo hakutaka kuthubutu kumtuma mwanawe wa mwisho wa Raheli.