# Masuke membamba Maneno "ya mbegu" inaeleweka. "Vichwa vyembamba vya mbegu" # yakayameza "wakala". Farao anaota ya kwamba mahindi ambayo hayana afya yanaweza kumeza mahindi yenye afya kama mtu anavyokula chakula. # masuke saba mema yote "vichwa vyenye afya na vizuri" # akaamka "aliamshwa" # tazama Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Farao alishangazwa na kile alichokiona. # ilikuwa ni ndoto "alikuwa akiota" # Ikawa Msemo huu unatumika kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. # roho yake ikafadhaika Hapa neno "roho" lina maana ya utu wake na hisia zake. "alifadhaishwa ndani ya utu wake" au "alisononeshwa" # Akatuma na kuwaita Inaeleweka ya kwamba aliwatuma watumishi. "Alituma watumishi wake kuwaita" au "Aliwatuma watumishi wake na kuwaita" # waganga na wenye hekima wote wa Misri Wafalme wa zamani na watawala walitumia wachawi na wenye hekima kama washauri.