# Tafsiri ni hii "Hii ndio maana ya ndoto" # Vikapu vitatu ni siku tatu "Vikapu vitatu vinawakilisha siku tatu" # atakiinua kichwa chako kutoka kwako Yusufu pia alitumia msemo huu "atainua kichwa chako" alipoongea kwa mnyweshaji katika 40:12. Hapa ina maana tofauti. Maana zaweza kuwa 1) "atainua kichwa chako na kuweka kamba katika shingo yako" au 2) "atainua kichwa chako kukikata" # mwili Hapa "mwili" una maana ya sehemu laini katika mwili wa mtu.