# Yusufu akaja kwao "Yusufu akaja kwa mnyweshaji na mwokaji" # Tazama, walikuwa na uzuni Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Yusufu alishangazwa na kile alichokiona. "Alishangazwa kuona ya kuwa walikuwa na huzuni" # maafsa wa Farao waliokuwa pamoja naye Hii ina maana ya mnyweshaji na mwokaji" # kifungoni katika nyumba ya bwana wake "Gerezani katika nyumba ya bwana wake". "Bwana wake" ina maana ya bwana wa Yusufu, kapteni wa walinzi. # Je tafsiri haitoki kwa Mungu? Yusufu anatumia swali kuonyesha msisitizo. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "tafsiri ni za Mungu!" au "Ni Mungu ambaye anaweza kusema maana ya ndoto!" # Niambieni, tafadhari Yusufu anawaomba wamumbie ndoto zao. "Tafadhali niambieni ndoto"