# Ikawa Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya tukio jipya la simulizi. # mnyweshaji Huyu ni mtu ambaye huleta vinywaji kwa mfalme. # mwokaji wa mfalime Huyu ni mtu ambaye alitengeneza chakula cha mfalme. # walimkosa bwana wao "walimkwaza bwana wao" # maafsa wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji ""mnyweshaji kiongozi na mwokaji kiongozi" # Akawaweka katika lindo katika nyumba ya kapteni wa walinzi "Akawaweka katika gereza liliokuwa katika nyumba ambayo ilisimamiwa na kapteni wa walinzi" # Akawaweka Mflame hakuwaweka gerezani lakini aliwaamuru wafungwe. "Akafanya wawekwe" au "Aliamuru walinzi wake kuwaweka" # katika gereza lile Yusufu alimofungwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hili lilikuwa gereza lile lile ambalo Yusufu alikuwemo" au "Hili lilikuwa gereza lile lile ambalo Potifa alimweka Yusufu"